📍 P.O. Box 511 Dodoma, Tanzania 📞 +255 757 100 888
Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Kristo (ASC)

Maria De Mattias Pre & Primary School

Tunanuia kuwapa vijana nafasi nzuri ya kukua kimaadili, kiali na kimwili chini ya misingi thabiti ya upendo na taaluma iliyotukuka.

Tuma Maombi / Uliza Maswali Soma Zaidi
Kauli Mbiu / Motto

"Elimu kwa kizazi chenye matumaini"

(Education for a future of hope)

Maadili na Malezi Bora

Kujenga msingi wa nidhamu, kiroho na upendo kwa kila mtoto bila ubaguzi.

Taaluma ya Juu

Kuhakikisha kila mwanafunzi anafikia ufaulu wa hali ya juu na kujitegemea.

Mazingira Jumuishi

Kuwasaidia na kuwajumuisha watoto wote pasi na ubaguzi kupata elimu na usawa kijamii.

Historia na Msingi wa Shule Ya Maria De Mattias

Shule ya Maria De Mattias imeanzishwa kwa kusudi la kuwapa vijana nafasi nzuri ya kukua kimaadili, kiali na kimwili.

Maria De Mattias, mwanzilishi wa Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Kristo (wanaomiliki shule), alikuwa na upendo mkuu kwa vijana. Aliamini kuwa kwa njia ya elimu kila kiumbe anaweza kumwelewa zaidi Mungu na maana ya maisha.

Upendo na Huruma Katika Malezi Masista wetu wanatumia kila mbinu ili vijana wajifunze, waelewe uwema, na wapendwe kwa huruma na kwa moyo wote.

Zaidi ya hayo, shule hii imejengwa kwa ajili ya kupokea watoto wote pasi na ubaguzi ili waweze kupewa elimu kama ufunguo wa maisha na kuwarejesha katika mazingira ya kawaida kijamii.

Taarifa Muhimu

  • Jina la Shule: Maria De Mattias Pre & Primary School
  • Anwani: P.O. Box 511 Dodoma
  • Ummiliki: Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Kristo
  • Mahali: Dodoma, Tanzania

Mwelekeo WETU KITAALUMA NA KIMAADILI

Tunaweka viwango vya juu vya mahadhurio, ufaulu na nadharia kwa mazingira halisi.

Dira (Vision)

Kutoa Elimu bora kwa watoto wote kwa kuhakikisha kila mtoto anafikia kiwango cha juu cha kuelewa na kufaulu ili aweze kujitegemea kimaadili, kiuchumi na kijamii kama nafsi na Taifa kwa ujumla.

Kauli Mbiu (Motto)

"Elimu kwa kizazi chenye matumaini"

(Education for a future of hope)

Malengo (Mission)

  • Kusimamia mahadhurio yawe 95% ya watoto wote kila siku katika shughuli zote za shule.
  • Kumsiadia mwanafunzi ajifunze kwa njia shirikishi kupata alama angalau 85% kwenye mazoezi na mitihani.
  • Kujenga uwezo wa kuoanisha nadharia aliyojifunza na mazingira anayoishi kwa kiwango cha 85%.

Pakua Fomu na Taarifa za Shule

Pata fomu za kujiunga na maelezo ya kina ya shule hapa.

School Prospectus 2026

Maelezo ya jumla kuhusu masomo, misingi na mazingira ya shule.

Pakua PDF

Fomu ya Maombi ya Udahili

Fomu rasmi ya kujiunga na Baby Class hadi Darasa la VII.

Pakua Fomu

Mawasiliano na Anwani

Tupo tayari kupokea maswali yako kuhusu usajili, nafasi za masomo na ushirikiano.

Maria De Mattias Pre & Primary School

P.O. Box 511 Dodoma, Tanzania

+255 757 100 888

Tuma Ujumbe Au Ulizo

Jaza fomu hii kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa usaidizi wa haraka.